Sera za TAPIFA

Sera ya faragha

Jinsi TAPIFA inavyokusanya, kutumia na kulinda taarifa binafsi za wanachama wake na za kila mtu anayetumia tapifa.co.tz.

Imesasishwa: 24 Novemba 2026

1. Sisi ni nani

Chama cha Wafugaji Nguruwe Tanzania (TAPIFA) ndicho kinachohusika na taarifa zako ("mdhibiti wa taarifa"). Shamba Manager inaendesha tovuti ya tapifa.co.tz na mfumo wa wanachama kwa niaba ya TAPIFA, na kwa maelekezo yake tu.

2. Taarifa tunazokusanya

Tunakusanya kile tu kinachohitajika kwa kila huduma:

  • Kujiunga na TAPIFA: jina lako, namba ya simu, mkoa, wilaya na kijiji; na ukipenda, barua pepe, jina la shamba, idadi ya nguruwe, na kama uliomba akaunti ya Shamba Manager.
  • Wanachama ambao TAPIFA ilikuwa nao tayari: ofisi ya TAPIFA inaweza kuwaingiza wanachama kutoka rejista yake (jina, simu, mkoa, wilaya, tarehe ya kujiunga na kama ada imelipwa). Wanachama hawa wanapata taarifa za TAPIFA kama waliojiunga kwenye tovuti.
  • Kulipa ada: kiasi, tarehe, mtandao wa simu na namba ya kumbukumbu ya malipo. Namba yako ya siri (PIN) na taarifa za pochi ya simu huenda kwa mtoa huduma wa malipo, kamwe si kwa TAPIFA.
  • Kuomba aina za nguruwe: jina, simu, mkoa na wilaya, idadi ya nguruwe unaotaka, na ujumbe wako.
  • Kutoa ofa kwa oda ya soko: idadi, uzito, lini watakuwa tayari, bei uliyotaja na ujumbe wako; na kama uliomba SMS za oda mpya.
  • Kutuandikia: jina lako, simu au barua pepe uliyotoa, na ujumbe wako.
  • Kwa usalama: anwani ya mtandao (IP) yako huhifadhiwa kama alama iliyochanganywa isiyoweza kurudishwa kuwa anwani, ili kuzuia fomu zisitumike vibaya.

3. Tunazitumia kwa nini

  • Kutunza rejista ya wanachama na kukupa namba yako ya uanachama.
  • Kupokea ada yako na kukuonyesha wewe na TAPIFA hali yake.
  • Kukutumia SMS kuhusu ada yako (vikumbusho kabla na baada ya mwaka wako kuisha), taarifa za chama na tahadhari za magonjwa.
  • Kujibu ujumbe wako na maombi yako ya aina za nguruwe.
  • Kuwaunganisha wafugaji na oda za wanunuzi: kuwatumia SMS wanachama walioomba taarifa za soko, na kukujulisha kama ofa yako imekubaliwa.
  • Kuhesabu wanachama, mashamba na mikoa kwa ripoti za TAPIFA, bila kumtaja mtu.

4. Kwa nini tunaruhusiwa kuzitumia

Kwa sababu ulikubali ulipojaza fomu, kwa sababu uanachama wako unazihitaji (ada yako, namba yako), na pale sheria inapoitaka TAPIFA kutunza kumbukumbu.

5. Nani anaziona

TAPIFA haiuzi taarifa zako wala kuwapa watangazaji. Ndani ya TAPIFA, ofisi na maafisa ugani huona wanachama wa eneo lao tu. Nje ya TAPIFA, ni huduma zinazofanya kazi husika tu, kila moja kwa kazi hiyo peke yake:

  • Shamba Manager, inayoendesha tovuti na mfumo wa wanachama.
  • Snippe, inayopokea malipo ya simu.
  • Africa's Talking, inayofikisha SMS.
  • Supabase, inayohifadhi hifadhidata, na Cloudflare, inayofikisha tovuti.

TAPIFA ikikubali ofa yako kwa oda ya soko, inaweza kumpa mnunuzi huyo jina lako, simu yako na mahali shamba lako lilipo, ili kupanga usafirishaji. Mnunuzi hapati chochote kuhusu ofa ambazo TAPIFA haikukubali.

TAPIFA hutoa taarifa kwa mamlaka ya serikali pale tu sheria inapotaka hivyo.

6. Taarifa zinazohifadhiwa nje ya Tanzania

Baadhi ya huduma hizi huhifadhi taarifa kwenye seva zilizo nje ya Tanzania. Zinalazimika kuzilinda na kuzitumia kwa huduma zao tu, kama Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya 2022 inavyotaka.

7. Tunazihifadhi kwa muda gani

  • Taarifa za uanachama: muda wote ukiwa mwanachama. Baada ya hapo, kwa muda tu ambao TAPIFA inazihitaji kwa kumbukumbu zake, na unaweza kuomba zifutwe wakati wowote.
  • Kumbukumbu za malipo: miaka mitano, kama sheria za kodi za Tanzania zinavyotaka.
  • Ujumbe na maombi ya aina za nguruwe: mpaka yashughulikiwe, kisha kwa muda tu ambao TAPIFA inahitaji kumbukumbu yake.
  • Ofa za oda za soko: kwa muda ambao TAPIFA inahitaji kumbukumbu ya oda na waliyoijaza.
  • Alama zilizochanganywa za anwani za mtandao: siku tisini, kisha hufutwa zenyewe.

8. Haki zako

Unaweza kuiomba TAPIFA:

  • ikuonyeshe taarifa inazokuhifadhia;
  • isahihishe kilichokosewa;
  • ifute taarifa zako (isipokuwa kumbukumbu za malipo za miaka mitano);
  • iache kukutumia SMS: tumia kiungo cha "Acha SMS" kwenye taarifa yoyote ya TAPIFA, au iambie ofisi;
  • iache kutumia taarifa zako kwa jambo usilokubaliana nalo.

Kama hujaridhika na jibu la TAPIFA, unaweza kulalamika kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) ya Tanzania.

9. Zinavyolindwa

Taarifa husafiri zikiwa zimefichwa (https). Ni walioingia kwenye mfumo wa TAPIFA tu wanaoweza kuona wanachama, na kila mmoja huona kile nafasi yake inaruhusu. Kila badiliko hurekodiwa pamoja na aliyelifanya.

10. Vidakuzi (cookies)

Tovuti inatumia kidakuzi kimoja tu chake yenyewe, kukumbuka lugha uliyochagua. Soma sera ya vidakuzi: tapifa.co.tz/vidakuzi

11. Mabadiliko

Sera hii ikibadilika, tarehe iliyo juu hubadilika. Badiliko likiathiri jinsi taarifa zako zinavyotumika, TAPIFA itawajulisha wanachama.

12. Mawasiliano

Kwa jambo lolote kuhusu taarifa zako: