Sera za TAPIFA

Sera ya vidakuzi (cookies)

Kidakuzi (cookie) ni faili dogo ambalo tovuti huhifadhi kwenye kivinjari chako. tapifa.co.tz inatumia vichache iwezekanavyo: hakuna vidakuzi vya matangazo, wala vinavyokufuatilia kwenye tovuti nyingine.

Imesasishwa: 24 Novemba 2026

KidakuziKazi yakeMudaAinaWapi
sm_tapifa_langHukumbuka kama ulichagua Kiswahili au Kiingereza.Mwaka 1Chaguo lakotapifa.co.tz na mfumo wa TAPIFA
__cf_bmHuwekwa na Cloudflare kutofautisha watu na mashambulizi ya kiotomatiki. Hakina chochote kuhusu wewe ni nani.Dakika 30Usalama (lazima)tapifa.co.tz
sb-…-auth-tokenHuwaweka watumishi wa TAPIFA ndani ya mfumo baada ya kuingia.Hadi atokeLazimaMfumo wa TAPIFA tu (admin.shambamanager.co.tz)

Hakuna ufuatiliaji wala matangazo

Tovuti haitumii Google Analytics, Facebook pixel wala huduma nyingine yoyote ya kufuatilia au matangazo. Ndiyo sababu haikuombi kukubali vidakuzi: vilivyo hapo juu vinahitajika ili tovuti ifanye kazi, au vinakumbuka chaguo ulilofanya.

Kuvifuta

Unaweza kufuta vidakuzi kwenye mipangilio ya kivinjari chako wakati wowote. Tovuti itaendelea kufanya kazi; itaonyesha Kiswahili mpaka uchague tena.

Taarifa zako

Jinsi TAPIFA inavyotumia taarifa zako binafsi: tapifa.co.tz/faragha